Francis Cheka kulia akitupa konde bila mafanikio baada ya Karama Nyilawila kulikwepa kwa ufundi katika mpambano wao uliofanyika mwisho wa mwiki iliyopita mjini Morogoro.
Karama Nyilawila kulia akimpa kitu cha kidevu bondia Francis Cheka na kujichukulia point katika pambano kali lililowakutanisha wikiendi iliyopita mji kasoro bahari na kumfanya Francis Cheka kuendelea kutamba kwamba hana mpinzani.
Francis Cheka kulia akimkatizia makonde ya mzunguko kijana Karama Nyilawila na kujikusanyia pointi za ushindi katika pambalo lao lililojaa upinzani mkali sana.
Mpaka mwisho wa mchezo Francis Cheka kulia alitangazwa kuwa ndiye mshindi kwa point zaidi ya Karama Nyilawila.Francis Cheka atangaza hakuna bondia wa kumpiga kwa Tanzania.