MWIMBAJI wa Kundi la Jahazi Modern Taarab, Khadija Yusuf, Januari 10, mwaka huu alijifungua kwa njia ya upasuaji lakini bahati mbaya mtoto wake alifariki dunia Januari 11 na kuzikwa siku hiyo katika makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mipango wa kundi hilo, Khamis Boha aliliambia chanzo cha habari hizi juzikati kuwa, Khadija ilikuwa ajifungue Machi, mwaka huu lakini alilazimika kufanyiwa upasuaji kutokana na kusumbuliwa na presha ya kushuka.

“Daktari wake alishauri afanyiwe upasuaji badala ya kusubiri mpaka Machi kwani amekuwa akisumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu. Upasuaji ulifanyika vizuri lakini bahati mbaya mtoto aliishi siku moja tu, akafariki na sikumbuki alikuwa jinsia gani,” alisema Boha.
Hii ni mara ya pili kwa mwimbaji huyo kupata tatizo kama hilo. Siku za nyuma aliwahi kujifungua lakini mtoto hakukaa siku nyingi, akafariki.