Na Shakoor Jongo
WIKI mbili zimekatika toka kuandikwa kwa habari ya mcheza sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel kumtosa aliyekuwa mpenzi wake, Mwilu Mwilola ‘Silva’, tayari kuna tetesi jamaa huyo ameanza kuangukia kwa demu wake wa zamani, Sarah Fred Mwakapala ‘Bukabi’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mara baada ya Aunt kumtema, Silva alianza kutuma meseji zenye mwelekeo wa kutaka kurudisha ‘majeshi’ kwa Bukabi licha ya kwamba aliwahi kumtenda vibaya mrembo huyo anayeshika nafasi ya 3 taji la Miss Utalii Mbeya, 2004.
Inadaiwa kuwa Bukabi amekuwa akirejesha meseji za Silva akimpasha kuwa hana mpango wa kumpa ‘second chance’ jamaa huyo.
Mwaka 2009, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Bukabi alimfumania Silva akiwa na Aunt kitandani tukio ambalo mrembo huyo alidai lilimuumiza kupita kiasi. Aunt alikana kutokea kwa tukio hilo licha ya vielelezo.
Tukio hilo liliripotiwa kwa mara ya kwanza kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi.
Amani, juzi Jumanne lilimsaka Bukabi kwa njia ya simu na kumuuliza kama ni kweli aliyekuwa mpenzi wake huyo anajigonga kwake.
“Mh! Nani kakwambia?”
Amani: “Jibu moja, kweli si kweli?
Bukabi: Ni kweli, jamaa ananitumia meseji, anadhani naweza kurudiana na yeye, thubutu yake. Alinipa machungu sana siku zile za fumanizi na Aunt, lakini sisemi sana si unajua nimezaa naye.”

0 Comments