Watu sita wa familia moja, Wakazi wa Kijiji cha Tumbe Wilaya Micheweni kisiwani Pemba, wamekufa na wengine sita kulazwa hospitalini baada ya kula nyama ya kasa.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kusini Pemba, Yahaya Rashidi Bugi amewataja waliokufa kuwa ni Sarah Hamadi Bakari (55); Zuwefa Omar Khamis (9); Aisha Saidi Juma (7); Fatuma Abdallah Rajabu (5); Mariamu Said Juma (miezi 5) na Nasiria Khatibu Haji (1.5) .
Bugi aliwataja walioathirika kwa kula kasa huyo na kulazwa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni kuwa ni Saidi Juma Khatibu (45), Rehema Bakari Simba (25), Mwanahamisi Bakar Mwinjabu (70), Saidi Juma Khatibu (20), Mkitu Haji Abeid (48) na Ziayana Juma Khatibu, wakazi wa kijiji hicho.
 |
Alisema kuwa kasa huyo alivuliwa baharini na mmoja wa watu hao waliolazwa hospitalini na kumchinja baada kurejea nyumbani kisha kugawa nyama yake na nyingine kuifanya kitoweo. Kwa mujibu wa Kamanda huyo, baada ya kuila nyama hiyo, watu walitapika na kuharisha na kukimbizwa hospitali kwa matibabu. Alisema waliokufa walikimbizwa katika Hospitali ya Cotege Micheweni kwa matibabu. Mvuvi wa kasa huyo na wenzake wawili wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini huku wenzao watatu wakiwa wameruhusiwa kurejea nyumbani kutokana na hali zao kuendelea vizuri. Afisa Mdhamini wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Kisiwa cha Pemba, alisema amewatuma maofisa wa afya kwenda katika Kijiji hicho kuchunguza kama kuna watu zaidi walioathiriwa na kasa huyo kwa kuwa inasemekana kuna zaidi waliokula
|
0 Comments