Akizungumza na chanzo cha habari hizi jana jijini Dar es Salaam, Rais wa chama hicho, Dk. Namala Mkopi,(pichani kushoto) alisema anashindwa kuelewa ni kwa nini serikali inashindwa kutumia busara katika kufanya maamuzi na matokeo yake kutumia mabavu kama ilivyotokea wakati wa mgomo wa Muhimbili.
Alisema kitendo cha serikali kuwahamisha madakatari hao na kuwapeleka katika hospitali za Wilaya ni kutaka kuwadumaza kitaaluma kwa kuwa hospitali nyingine hazina madaktari bingwa.
Dk. Mkopi alisema serikali ilitakiwa kuliangalia suala hilo kwa kina zaidi kuliko kufanya kwa lengo la kuwakomoa madaktari.
Alisema katika mkutano wao ambao utawakutanisha madaktari wote wa nchini unatarajia kufanyika kesho ambapo pia watajadili suala hilo la madaktari kuhamishiwa katika hospitali za Wilaya pamoja na mambo mengine ambayo yamejitokeza.
Hata hivyo, alisema kwa kuwa kikao hicho ndicho kitaamua maamuzi juu ya sakata hilo na kwamba kwa sasa hawahitaji kufanya malumbano na serikali.
Alisema taaluma hiyo inatakiwa kuheshimiwa na sio watu kuidharau kwani imekuwa ikihitajika kwa asilimia kubwa na jamii hapa nchini kwenye mataifa mengine.
Dk. Mkopi alisema amepatiwa taarifa kuwa madaktari 150 wamebakishwa katika hospitali ya Muhimbili hapo na wengi kuhamishiwa katika hospitali za Wilaya.
0 Comments