Rais Barrack Obama amekiri bayana kuwa jeshi la Marekani linatumia ndege za kivita zizizokuwa na rubani kulenga washukiwa wa wapiganaji wa kiislamu wa al Qaeda katika maeneo ya kiukoo nchini Paksitan.
Rais Obama amesema hayo wakati wa kikao kilichoandaliwa na kampuni ya huduma za tovuti ya Google.Mashambulio ya kutumia ndege hizo za kivita yamekuwa mbinu kuu ya kupambana na wapiganaji wa al qaeda nchini afghanistan na Pakistan.
Kama sheria utawala wa rais obama haujadili mashambulio ya anga yanayotekelezwa na ndege za kivita zizizokuwa na rubani hadharani.
Na operesheni ya jeshi la marekani nchini Pakistan imekuwa jambo la siri.
Kwa hivyo imekuwa ni jambo la kushangaza kusikia rais mwenyewe akijitokeza, na kusema kuwa kumekuwa na mashambulio mengi katika maeneo ya kiukoo nchini Pakistan karibu na mpaka wa Afghanistan.
Rais Obama alikuwa ameulizwa kuhusu suala la raia waliojeruhiwa au kuuawa kwenye operesheni hiyo na ikiwa mashambulio hayo ya Marekani yamekiuka uhuru wa Pakistan.
Lakini rais Obama alijibu akisema, hilo ni suala ambalo lilikuwa limepangwa vilivyo, silaha zinazoaminika na ambazo matumizi yake, kwa mujibu wa matamshi yake yamewekwa kuwa siri ya hali ya juu.
Rais Obama amesema kutokana na hali duni ya miundo msingi katika maeneo hayo ya kiukoo nchini Pakistan, iwapo mbinu nyingine ingelitumika kupambana na wapiganaji wa al qaeda, ingelikiuka zaidi uhuru wa Pakistan.
0 Comments