Matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa wabunge wa Misri yametangazwa.
Yanathibitisha kuwa chama cha Muslim Brotherhood ndicho kilichopata viti vingi kabisa.
Tume ya uchaguzi ilisema kuwa chama hicho kimepata asili-mia-38 ya viti vya vyama, na karibu asili-mia-50 ya viti vyote.
Chama cha Kiislamu cha msimamo mkali kilikuwa cha pili, na hivo kuvipa vyama vya Kiislamu, karibu thuluthi-mbili za viti vya bunge.
Uchaguzi huo uliofanywa katika duru tatu, ndio wa kwanza, tangu Rais Mubarak kulazimika kung'atuka baada ya maandamano makubwa.