Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Dkt. Wilbrod Slaa usiku wa jana Ikulu jijini Dar es salaam wakati Uongozi wa chama hicho ulipofika kukutana na Rais kwa muendelezo wa mazungumzo ya mchakato wa Katiba mpya.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Dkt. Wilbrod Slaa (kushoto) akifafanua jambo kwa Rais Jakaya Kikwete kuhusu mchakato wa Katiba Mpya ikulu Jijini Dar es Salaam jana.Katikati ni Mwenyekiti wa Chama hicho,Mh. Freeman Mbowe.
Rais Jakaya Kikwete akiukaribisha Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) usiku wa jana Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akiongea na uongozi wa NCCR-MAGEUZIMkuu wa Idara ya Katiba na Sheria wa Chama cha NCCR - Mageuzi, Dk. Sengondo Mvungi akisoma mapendekezo ya chama hicho juu ya mchakato wa katiba.
Rais Jakaya Kikwete akipokea mapendekezo ya chama cha NCCR-MAGEUZI kuhusu mchakato wa Katiba toka kwa Mwenyekiti wa chama hicho Mh James Mbatia jana alipokutana na uongozi wa chama hicho Ikulu jijini Dar es salaam.
Jakaya Kikwete akiagana na Viongozi wa NCCR-MAGEUZI mara baada ya picha ya pamoja.Picha na Ikulu.