Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne,kwanza Watu,pili Ardhi,Siasa safi na Uongozi bora.Kumbuka iwe kiongozi wangu huyu alipokupa kura yake alitegemea mabadiliko ya maisha yake kupitia wewe,sasa unapojifanya huoni tatizo kama hili unakuwa umekiuka moja ya mikataba ya kauli yako ulizotoa kipindi kile cha kusaka kura.Iwe Diwani, Mkuu wa Wilaya,Mbunge,Mkuu wa Mkoa sio kila kitu afanye rais kwani wewe ndiye uliye karibu na mwananchi wako,fanya kile ulichokiahidi kukifanya usisubiri kipindi cha mwisho ukaombe kura ya mnyonge kwa kumdanganya tena na staili zako.Huu ni wangu ushauri tafadhali msinihukumu japo ukweli unauma.