Mshiriki wa Tanzania katika shindano la Miss Tourism Queen International 2011, Nelly kamweli amefanikiwa kushika nafasi ya 5 katika shindano hilo lilifanyika Desemba 29, 2011 katika kituo cha Kimataifa cha Maonesho wa Qujiang uliopo mji wa Xi'an, China. Taji hilo lilienda kwa mshiriki kutoka Vietnam, nafasi ya pili ikienda Ufilipino, tatu ikienda nchini Thailand ambapo nafasi ya nne ilichukuliwa na kimwana kutoka Nchini Australia.(na fk) 
 Nelly (wapili kushoto) akiwa na washiriki wenzake jukwaani.