Msanii Diamond akiwa chini ya ulinzi wa wazee wa kazi(Polisi)akitolewa hotelini alikupangiwa na kupelekwa kituo cha polisi baada ya kumshambulia kamanda wa matukio mkoani Iringa bwana Francis Gondwin.
Kamanda wa matukio mkoani Iringa bwana Francis Godwin akionyesha jacket lilivyochanwa na msanii Diamond baada ya kushambuliwa katika uwanja wa Samora mjini Iringa. 
Msanii Diamond ameruhusiwa kudhaminiwa leo majira ya saa 6 mchana na kuondoka kuelekea jijini Dar es Salaam kufanya uzinduzi wa Albamu yake,msanii huyo aliwekwa mahabusu ya kituo cha polisi mjini Iringa kwa tuhuma za kumpiga na kuharibu vitendea kazi vya mmiliki wa mtandao  wa www.francisgodwin.blogspot.com uwanja wa Samora mjini Iringa