Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, kuhusu kuahirishwa kwa Mjadala wa Shirika la Maendeleo ya Mafuta nchini(TPDC) ambao utaenda kujadiliwa kwenye Kikao kijacho cha Bunge. Picha na Zacharia Osanga.


Patricia Kimelemeta na Fidelis Butahe
KAMATI ya Hesabu za Mashirika ya Umma(POAC), imeshindwa kujadili suala la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) kutokana na baadhi ya makampuni kukataa kutoa fedha za mafunzo kwa watalaam wa fani ya mafuta.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe alisema hayo juzi jijini Dar es Salaam kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari.

Zitto alisema kuwa, kila Kampuni inayochimba mafuta nchini inatakiwa kutoa kiasi cha Sh1.8 bilioni kwa ajili ya kuwawezesha watanzania kupata mafunzo hayo bila ya kuangalia ni nani na kwamba ana maslahi gani kwa taifa, kutokana na hali hiyo wananchi wanapaswa kujitokeza kusoma masomo hayo ili waweze kunufaika na mafunzo hayo.

Aliongeza kutokana na hali hiyo watanzania wanapaswa kutambua kuwa, makampuni yanayowekeza katika mafuta yana mchango gani kwa wananchi na jinsi ya kunufaika nayo.

Alisema mbali na hilo pia kamati imewataka TPDC kupeleka mchanganuo wa ujenzi wa bomba La mafuta kutoka Mtara hadi Dar es Salaam ili waweze kuangalia gharama zitakazotumika wakati wa kukamilika kwa mradi huo.
Alisema kutokana na hali hiyo, bomba hilo litaweza kusafirisha mafuta na kusambaza mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya matumizi