Ni Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Pia, ni Beyonce yuleyule mwimbaji maarufu duniani ambaye ni Mmarekani.
Akiwa na mumewe Jay Z, mrembo Beyonce ambaye jina lake kamili ni Beyonce Gissele Knowles waliitembelea Tanzania “kinyemela” wakati walipofungua visima maalum vya maji katika harakati za mradi wa kimataifa kuwapatia wanadamu maji.
Hiyo ilikuwa Oktoba 2006.

Mwanamke huyo mwenye kuvutia katika kila idara na maarufu kwa uimbaji, utunzi wa nyimbo na kurekodi nyimbo (prodyuza) na ambaye jina lake lenye asili ya Kifaransa hutamkwa “Biyonse”, ndiye yuleyule ambaye hivi sasa kwa wapenda muziki wanafuatilia kwa makini habari za mtoto wake ambaye amejifungua hivi karibuni. Mtoto huyo wa kike anaitwa Ivy Blue Carter.
Mume wa Beyonce naye ni mmoja wa wanamuziki mastaa duniani ambaye jina lake halisi ni Shawn Carter.
Ziara yao hiyo ambayo haikutangazwa sana kwa sababu ambazo hazikujulikana, iliwashitua wengi baada ya kuwaona wanamuziki hao mashuhuri duniani wakiwa wanavinjari mitaa ya Mwananyamala, wakiwa wamekaa kwenye mkutano na kwenye meza ya kawaida ambayo waliwekewa soda zilizotengenezwa Tanzania.