Mkuu wa huduma za misaada za Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Mark Bowden, ameiambia BBC kwamba watu zaidi watakufa kwa sababu ya njaa, kabla ya utapia mlo kudhibitiwa.
Ingawa hali inatengenea lakini Wasomali 250,000 bado wana njaa, na shida hizo zitaendelea hadi mwezi wa Julai au Agosti.
Bwana Bowden alisema njaa imeuwa maelfu kadha tangu ilipotangazwa miezi sita iliyopita; utapia mlo mkubwa kati ya watoto umeripotiwa Somalia, na nusu ya watoto wanatapia mlo.
(Toka bbc)
0 Comments