Mtangazaji mahiri wa Clouds FM kupitia kipindi cha Leo Tena,Dina Marios (pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge mbalimbali wa viti maalum,mara baada ya kuzungumza nao machache kuhusiana na harambee ya kuisaidia/kuiwezesha timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars),ishinde katika mchezo wao wa marudiano wa kuwania kufuzu Fainali Afrika kwa Wanawake (AWC),unoatarajiwa kufanyika hivi karibuni dhidi ya timu ya Namibia.

Aidha katika mpambano huo viingilio vimetajwa kuwa ni sh 10,000 kwa VIP A,Sh 5,000 kwa VIP B na C,huku sh 3,000 ikiwa kwa jukwaa la orange na sh 2000 kwa jukwaa la blue.Kama vile haitoshi Wabunge hao na wengineo kesho watakuwa na mechi ya kirafiki kwenye uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuihamasisha jamii kwa namna moja ama nyingine kuiwezesha timu ya Taifa a.k.a Twiga Stars.
Kutoka kulia ni Mbunge wa viti Maalum (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mh. Ummy Ally Mwalimu,Wa tatu kulia ni Mbunge wa Viti Maalum CCM,Mh Vicky Kamata,Mbunge Viti Maalum Mh.Zainab Kawawa,Mh.Grace Kiwhelu Mbunge viti maalum CHADEMA pamoja na Mh.Zaynab Matitu Vulu ambaye ni Mbunge viti maalum CCM.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Bw. Joseph Kusaga akizungumza machache na baadhi ya Wabunge wa viti maalum mara baada ya kumaliza mahojiano yao mafupi kupitia kipindi cha Power Breakfast na Leo Tena ndani ya Clouds FM mapema leo,Mikocheni jijini Dar.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM),Mh.Zaynab Matitu Vulu akifafanua jambo mapema leo ndani ya Clouds Fm kupitia kipindi cha Leo Tena,kuhusiana na mchakato mzima wa kuiwezesha timu ya Taifa Wanawake a.k.a Twiga Stars iweze kufanya vyema kwenye mchezo wake unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni hapa jijini Dar.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM),Mh.Zainab Kawawa (kati) akiwataka wananchi mbalimbali kujitokeza kwa wingi hiyo kesho kwenye mchezo wao wa Wabunge dhidi ya Twiga Stars,ikiwa ni sehemu ya mchakato mzima wa kuiwezesha timu ya Taifa Wanawake a.k.a Twiga Stars iweze kufanya vyema kwenye mchezo wake unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni hapa jijini Dar.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM),Mh.Vicky Kamata na Mwenyekiti wa Victoria Foundation akisisitiza zaidi kujitokeza kwa wingi kwa wananchi mbalimbali hiyo kesho kwenye mchezo wao wa Wabunge dhidi ya Twiga Stars,ikiwa ni sehemu ya mchakato mzima wa kuiwezesha timu ya Taifa Wanawake a.k.a Twiga Stars iweze kufanya vyema kwenye mchezo wake unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni hapa jijini Dar.(Issa Michuzi)