Takriban watu ishirini na wanne wameuawa katika mji mkuu wa Baghdad nchini Iraq katika mashambulio kadhaa ya mabomu ya kutegwa garini na ardhini kutekelezwa.
Mashambulio hayo yametokea katika eneo la waislamu wa-Shia mjini humo ikiwemo eneo lenye umasikini mwingi la Sadr mjini humo.Waziri wa masuala ya ndani nchini humo anasema waathirika wote walikuwa raia. Watu wengi zaidi wamejeruhiwa.
Mwandishi wa BBC nchini humo anasema kuwa kumekuwa na ongezeko la machafuko ya kidini tangu kutolewa kwa kibali cha kukamatwa makamu wa Rais Tariq al-Hasimi,ambaye ni msunii kwa madai ya ugaidi mwezi jana.

0 Comments