Mahakama mjini London imewahukumu kifungo cha miaka 15 na miaka 14 wanaume wawili waliopatikana na hatia ya kumuua mvulana mweusi Stephen Lawrence.(Mvulana aliyeuliwa ni huyo pichani juu kushoto na wauaji ni hao hapo juu kulia).
Gary Dobson, mwenye umri wa miaka 36 na David Norris mwenye umri wa miaka walipatikana na hatia ya kumuua Lawrence Kusini mwa London, mwaka 1993.
Dobson atatumika kifungo kisichopungua miaka 15, naye Norris atakaa jela muda usiopungua miaka 14 na miezi mitatu.
Jaji Justice Treacy amesema hakusa sababu nyingine ya mauaji hayo ila chuki za ubaguzi.
Jaji huyo amesema huku hiyo ni ndogo kuliko ilivyotarajiwa, kwa kuwa wanaume hao walikuwa wa umri wa chini ya miaka kumi walipomuuwa Lawrence kwa kumchoma kisu.
Amesema uhalifu huo ulilitia doa taifa la Uingereza.
Upande wa mashtaka ulitegemea ushahidi uliotokana na uchunguzi mwingine, baada ya kesi ya kwanza iliyowasilishwa mahakamani na familia ya Lawrence dhidi ya wanaume watatu akiwemo Dobson, kutupiliwa mbali.
Wataalamu wa uchunguzi wa damu na alama kama hizo waligundua alama ya damu kwenye koti la Dobson ambalo bila shaka halingepatikana bila kumkaribia marehemu.
Kuanza upya kwa kesi hiyo kulileta mabadiliko makubwa katika uhusiano baina ya watu weusi na wazungu nchini Uingereza.
Wazazi wa marehemu Stephen, Doreen na Neville, waliangua kiliyo jopo lilipotangaza kua watuhumiwa wamepatikana na hatia.
Mamake Dobson, Bi.Gary Dobson, aliyeiambia mahakama kua mwanawe alikua nyumbani wakati wa mauwaji, aliangua kilio mahakamani kufuatia tangazo la watuhumiwa kupatikana na hatia.pelelezi wa kwanza uliofanywa na polisi ulishindwa na kupelekea Polisi ya mji wa London kutuhumiwa kama Idara inayoendesha ubaguzi wa rangi.
Stephen Lawrence alikua mwenye umri wa miaka 18 alipouawa kwa kisu akiwa karibu na kituo cha basi cha Eltham, London ya kusini mnamo mwezi April mwaka 1993.
Polisi walitambua watu watatu ambao baadaye walitajwa katika ripoti ya uchunguzi kama washukiwa wakuu.
Hadi wakati huo kulikuwepo mfululizo wa mapungufu ya polisi kwa kushindwa kukusanya ushahidi wa kutosha mara mbili, wa kwanza uliowasilishwa na wazazi wake Stephen Lawrence, Doreen na Neville Lawrence.
Lakini katika kuichunguza kesi hiyo kwa mda wa miaka minne, wataalamu wengine wa kupeleleza ushahidi waliweza kugundua ushahidi ulioweza kuwaunganisha washukiwa na mauwaji - ushahidi ambao ulia mikononi mwa polisi kwa kipindi kirefu.
Ushahidi huo wa alama za damu, nyuzi za nguo na unywele wa marehemu - vilipatikana kwenye nguo za washukiwa zilizotekwa tangu mwaka 1993.
Wataalamu wa upelelezi wa ushahidi walifanikiwa kugundua ushahidi huo kwa kutumia mitambo ya kisasa ambayo wakati ule havikuwepo.
Dobson, mwenye umri wa miaka 36, na Norris,akiwa na umri wa miaka 35, walikanusha madai ya kuua. Walidai kuwa damu hiyo ilichanganyika na nguo zao kutokana na kuchanganywa na ushahidi kupitia kipindi cha miaka mingi.
Wapelelezi walitumia muda kuchunguza jinsi ushahidi huo ulivyozungushwa na jinsi ulivyohifadhiwa kuondoa shaka ya uwezekano wa kuchanganywa kama walivyodai watuhumiwa.
Gary Dobson alikamatwa na kufungwa jela mnamo mwaka 2010 kwa kushiriki biashara ya kuuza mihadarati. Yeye ni miongoni mwa kundi dogo la wanaume waliohusishwa na uhalifu mmoja baada ya Mahakama ya rufaa kuzima ombi lake la rufani mnamo mwaka 1996.
0 Comments