Na Issa Mnally
KUDAADEKI! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kuona au kusikia sakata la Askari wa Kituo cha Polisi cha Magomeni jijini Dar es Salaam, kumnasa mke wa mtu akiwa gesti na raia wa kigeni.
Stori iko hivi, askari hao wakiwa kwenye majukumu yao ya kila siku, walitonywa juu ya kuwepo kwa raia huyo (jina lake halikufahamika mara moja) ambaye amekuwa ‘akimbonji’ katika nyumba hiyo ya kulala wageni iliyopo Manzese, Dar es Salaam bila kujua kuwa yupo nchini kihalali au la.
Baada ya askari hao kutonywa juu ya taarifa za raia huyo anayedaiwa ni Mbangaladeshi, juzi (Jumanne) saa tano usiku, walivamia katika nyumba hiyo na kwenda moja kwa moja katika chumba alichokuwa raia huyo na kumkuta na mwanamke huyo ‘wakijivinjari’.
Hata hivyo, jamaa huyo aliweza kusawazisha mambo kwa kutoa vibali vya muda vinavyomwezesha kuishi kihalali Bongo na kudai kuwa hati yake ya kusafiria ilikuwa ikishughulikiwa.
Baada ya askari hao kuhakikisha kuwa raia huyo alikuwa akiishi kihalali, walimwachia huru.
“Tumeridhika na vibali vyako, jitahidi kukamilisha taratibu nyingine, tunashukuru kwa ushirikiano wako, pumzika salama. Taarifa ambazo tulizipata ndizo zilizotufikisha hapa,” alisema mmoja wa maaskari hao wakati wakimuachia huru jamaa huyo.
Baadhi ya raia wema ambao walikuwepo wakati zoezi hilo likiendelea, walidai kuwa mwanamke aliyekuwa chumbani na Mbangaladeshi eti ni mke wa mtu.
“Yule mwanamke namjua, ni mke wa mtu, anaitwa Teddy na anaishi maeneo ya Magomeni, ila dah!” alisikika akisema mmoja wao.
0 Comments