Na Mwandishi Wetu
Katika hali ya kushangaza, msanii wa filamu Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ hivi karibuni alipiga picha huku akiyanadi matiti yake ambayo baadhi ya watu wanadai ni ya Kichina.
Picha ya msanii huyo ambayo inapatikana mtandaoni inamuonesha mwanadada huyo akiwa amepozi huku mikono yake ikiwa imeshusha chini ya sidiria na kuyaacha wazi matiti yake.
Aidha, maelezo yanadai Jack ‘alijivua nguo’ alipokuwa akionesha moja ya ‘tatuu’ zake inayopatikana kifuani ambapo katika kufanya hivyo aliianika sehemu yake hiyo nyeti.Alipotafutwa kuzungumzia sababu ya kupiga picha hiyo ambayo iko kinyume na maadili ya Kitanzania, msanii huyo hakuweza kupatikana mara moja ila baadhi ya watu walioiona picha hiyo walisema, amejidhalilisha.“Huu ustaa unawapeleka pabaya, sasa kupiga picha kama hii ndiyo nini kama siyo kutaka kuwadhalilisha wanawake wenzake? Ingekuwa matiti yenyewe ni halisi basi, kumbe ya Kichina,” alisema Mama Mariam wa Magomeni Dar.
0 Comments