Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akiongoza kikao cha Kamati ya uongozi ya bunge mara baada ya kipindi cha maswali na majibu Bungeni Dodoma jana. kamati ya Uongozi imekaa kupitia upya ratiba ya mkutano wa Bunge ulioanza leo kwa lengo la kuboresha na kupanga siku ya kujadili miswada mbalimbali itakayowasilishwa Bungeni. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge