Na Richard Bukos BOSI wa kundi la muziki wa mwambao la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’ amenaswa laivu bila chenga akiwa katika pozi la mahaba na mwanamuziki wa Bendi ya Mashujaa, Raja Ladha, Chanzo cha habari hizi linabumbulua.
Kwa muda mrefu, Isha baada ya kuachana na mume wake, Jumanne Hassan ‘Tevez’, hajaweka wazi anajiweka kwa nani hadi alipobambwa na kamera ya gazeti hili.

NI WAPI?
Tukio hilo lililoshuhudiwa kwa macho mawili ya paparazi wetu lilichukua nafasi Alhamisi iliyopita, katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar ambapo kundi zima la Mashauzi Classic lilikuwa likiwasha moto wa burudani.
Hatua ya kwanza ilikuwa ni mwandishi wetu kuwafotoa picha fasta ili kuweka ushahidi mkononi kabla ya kusaka upande wa pili wa habari ambapo Isha alitoa ushirikiano wa kutosha.

ENHEE! NI NANI WAKE?
Zoezi la picha lilipokamilika, mwandishi wetu alizuga kiana halafu baadaye akawafuata na kuwauliza uhusiano uliopo kati yao kiasi cha kujiachia kiasi kile.
Isha ndiye aliyekata mzizi wa fitina kwa kuweka mambo hadharani, msikie mwenyewe: “Huyu ndiye mpenzi wangu wa dhati, kiukweli ninampenda kwa moyo wangu wote.
“Nimechoshwa na longolongo za vijana hasa hawa wa Kibongo, hawana maana hata kidogo. Hata wakipendwa vipi, hawapendeki.”
 Chanzo cha habari: Unaposema umechoshwa na longolongo za vijana wa Kibongo, unamaanisha huyu siyo Mbongo?
Isha: Ndiyo...ni Mkongo, kwani humuoni alivyo handsome?
Chanzo cha habari: Kwa hiyo, unamaanisha sisi vijana wa Kibongo si watanashati?
Isha: (Alicheka sana, kisha akainuka na kupanda jukwaani).

TUJIKUMBUSHE
Isha aliwahi kuwa ndani ya ndoa na Tevez lakini waliachana kwa msanii huyo kupewa talaka.
Baada ya kuachana huko, Tevez aliripotiwa kuoa mwanamke mwingine lakini Isha hakusikika, hadi alivyofunguka juzi baada ya kunaswa akiwa na Raja.