Na Musa Mateja
Kifo cha malkia wa muziki wa Pop, RnB na Soul wa Marekani, Whitney Elizabeth Houston kilichochangiwa na matumizi ya madawa ya kulevya, kimeibua mapya ambapo listi ya mastaa wa Kibongo wanaodaiwa kutumia madawa hayo yakiwemo ‘unga’, bangi, mirungi na mengine imetajwa, chanzo cha habari kina ripoti kamili.
Habari za chini kwa chini zinadai kuwa kwa sasa mastaa kibao wanatumia madawa ya kulevya huku majina makubwa kama Msafiri Sayai ‘Diouf’, Albert Mangwair, Langa Kileo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, Waziri Makuto ‘Lord Eyez’, Fareed Kubanda ‘Fid Q’, Aisha Mbegu ‘Madinda’, Khaleed Mohamed ‘TID’, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’, Abas Kinzasa ‘20%’, David Nyika ‘Daz Baba’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Happiness Thadei ‘Sister P’ na Rose Ndauka yakitajwa.
“Chondechonde, tuungane kuwakanya mastaa wetu kwani wataondoka bado tukiwa tunawahitaji kama alivyoondoka Whitney na miaka 48. Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki tulindane na janga hili kwani litawamaliza vijana wetu ambao ndiyo nguvu kazi,” ilisomeka barua pepe iliyotumwa kwenye gazeti hili mwanzoni mwa wiki hii.
Baada ya kuinyaka listi hiyo, timu yetu ilizungumza na baadhi ya mastaa hao ambapo walikuwa na haya ya kusema.
Fid Q: Sijawahi kuvuta unga katika maisha yangu ila niliwahi kufanya kazi na shirika binafsi linaloitwa Rafiki Family lililokuwa likihamasisha watumiaji wa madawa ya kulevya waache na nilifanikiwa kutibu wawili nikiwa kama mwanamuziki maarufu.
TID: Hayo ni madai tu, sijihusishi kwa namna yoyote na madawa ya kulevya, watu wanasema tu kwa sababu mimi ni staa, ninayependa maendeleo na familia yangu, isitoshe siku zote mtafutaji hakosi kashfa.
20%: Kusema kweli unga hapana zaidi ya siku moja nilikwenda sehemu kupiga shoo nikakuta msanii mmoja aliyekuwa anajifanya ananifahamu sana, akawa anipakazia kuwa natumia unga, jambo ambalo si la kweli, ingawa mimi ninatumia bangi kweli na hilo sikufichi, lakini mbele ya watu huwa napenda kuzugia na bia.
BANZA STONE
Mwanamuziki huyo aliwahi kukiri kuwa alibobea kwenye matumizi ya unga lakini kwa sasa ni mtu safi.
AISHA MADINDA
Hivi karibuni alimtaja mwanamuziki aliyemsababisha akaingia kwenye janga hilo na kuapa kwamba kama siyo kuacha, leo asingekuwa juu ya uso wa dunia.
LANGA
Kwa sasa Langa anasema yeye ni ‘mtoto mzuri’ kwani ameamua kuacha hivyo kuwaomba vijana wenzake kutotumia ‘mambo hayo’ kwani ni kujitakia kifo.
DIOUF
Staa huyo aliwahi kudaiwa kutopea kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, hivi karibuni alilamba uongozi katika mradi wa kuokoa watu wanaotumia madawa ya kulevya katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mastaa wengine wa muziki wa kizazi kipya ambao wamekuwa wakikanusha ishu hiyo ni Mangwea, Ray C, Lord Eyez, Daz Baba na Sister P.
SHILOLE
Mwanadada huyo aliwahi kunaswa akitafuna mirungi ambapo alikiri kuwa ni sehemu ya ulevi wake.
Afande Sele na Jack wa Chuz walipotafutwa kupitia simu zao hawakupatikana.
0 Comments