Viongozi wa Somalia wametia saini mkataba ambao wanataraji utamaliza msuko-suko wa nchi hiyo.
Inaazimiwa kuwa na bunge jipya litalokuwa na baraza la pili la wazee na serikali za majimbo.
Wanawake watakuwa asili-mia-30 ya wabunge.
Makubaliano hayo yaliyotiwa saini na serikali ya sasa, utawala wa majimbo mawili, na wanamgambo wanaounga mkono serikali, yatajadiliwa juma lijalo, kwenye mkutano wa London kuhusu Somalia.
Lakini kundi la wapiganaji wa Kiislamu, al-Shabaab, ambalo linadhibiti sehemu kubwa ya kati na kusini mwa nchi hiyo, hawakushiriki kwenye makubaliano hayo.
0 Comments