Makamu mwenyekiti wa chama cha ngumi za kulipwa nchini, Madaraka Nyerere (kushoto), akiwaelekeza mabondia Francis Cheka (kulia) na Mada Maugo jinsi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kupigania ubingwa shirikisho la ngumi duniani (IBF) katika pambano la raundi 12, na litakalofanyika ukumbi wa PTA Saba Saba jijini Dar es Salaam tarehe 28 Aprili mwaka huu. Hafla hiyo ilifanyika leo jijini Dar.
Bondia Francis Cheka (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu mkataba huo.
Bondia Mada Maugo akiongea na waandishi wa habari (hawako pichani) katika hafla hiyo.Picha na super D.