Leo wakati naenda kufanya usafi wa miti nyuma ya nyumba ninapoishi nikacheka peke yangu pale nilipokutana na baadhi ya matunda yaliyobaki mtini.kwa kuwa nipo mbali na Afrika sikushangaa ustaarabu wa watu weupe ila nilikumbuka kwetu kuhusu haya matunda,nikajiuliza hivi yangekuwa mitaa ya Mbagala haya matunda yangebaki hivi juu ya mti? jibu lililokuja kichwani mwangu ni kwamba hapana....basi nikaendelea na shughuli zangu.