Jiwe linalosadikiwa kutumika katika mauaji ya marehemu Kasto.
WIMBI la kuuawa madereva wa pikipiki linazidi kushika kasi mkoani Morogoro ambapo usiku wa kuamkia leo dereva mwingine wa usafiri huo ambao unajulikana kama ‘bodaboda’ aliyefahamika kwa jina moja la Kasto, ameuawa kikatili kisha kuporwa pikipiki yake, kunyofolewa macho na kutupwa kwenye mashamba ya eneo la Chamwino katika Manispaa ya Morogoro.
Mtandao huu ulifika eneo la tukio na kushuhudia umati wa watu wakiwemo wanafunzi wa shule ya msingi wakijaribu kumtambua marehemu huyo ambapo baadhi ya watu walimtambua kwa jina la Kasto wakisema alikuwa akifanya biashara hiyo ya bodaboda kwenye kijiwe cha Tupendane jirani na nyumbani kwa aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) Omar Mahita.
Wauaji wa mtu huyo waliyanyofoa macho yake kwa lengo la kupoteza ushahidi wakihofia wangeweza kuonekana kwenye mboni za marehemu huyo.
Takribani mwezi mmoja uliopita dereva mwingine wa bodaboda aliuwawa kikatili na kuporwa kipikiki yake maeneo ya Kichangani katika Manispaa ya Morogoro.
NA DUNSTAN SHEKIDELE, MOROGORO
0 Comments