Na Walusanga Ndaki
MUUNGANO wa Wanaharakati wanaotetea usawa wa kijinsia, haki za binadamu na ukombozi wa wanawake kimapinduzi (FemAct) umeitaka serikali kufuta mashitaka dhidi ya wanachama wake waliokamatwa Februari 9 mwaka huu kuhusiana na kuitaka serikali imalize mgomo wa madaktari nchini.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa majuzi na taasisi hiyo inayojumuisha asasi za kiraia zipatazo 40, na kusainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na Sekretariat ya FemAct, Usu Mallya, ilieleza kwamba waliohusika ni wafanyakazi wa ituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wakati wanaelekea Hospitaliya Taifa ya Muhimbili kwenye kusubiri hatma ya mazungumzo kati ya Waziri Mkuu na madaktari kutoka hospitali za umma waliokuwa wamegoma kushinikiza madai yao ya muda mrefu kazini.
Taarifa hiyo imetoa namba za simu, faksi na barua pepe ikiwataka Watanzania kuwasiliana na ofisi za Waziri Mkuu, Inspekta Jenerali wa Polisi, Mkurugenzi wa Mashitaka, Waziri wa Masuala ya Kikatiba, Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai (RC)) na Wizara ya Mambo ya Ndani iwaachie mara moja waliokamatwa na iache kuwanyanyasa wananchi wanadai haki zao.
Wafanyakazi hao walikamatwa na kufunguliwa mashtaka eti kwa kosa la kufanya mkusanyiko haramu.
Taarifa hiyo ilitaja miongoni mwa waliokamatwa kuwa ni wafanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Mkurugenzi Mtendaji, Dk. Helen Kijo-Bisimba, Anna Migila, Marcus Albany na Godfrey Mpandikizi; na Ananilea Nkya, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi Habari Wanawake Tanzania (TAMWA).

Wengine ni Irenei Kiria, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la SIKIKA; wafanyakazi na wanachama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakiwemo Dk. Diana Mwiru, Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Jinsia, Anna Kikwa, Mkuu wa Idara, Utawala na Fedha na Dorothy Mbilinyi, Afisa Mwandamizi wa Programu, Ukuzaji wa Mitaala na Mafunzo, Taasisi ya Mafunzo ya Jinsia.
Pia wamo wajumbe kutoka vikundi na mitandao ya kijamii, wakiwa ni pamoja na: Specioza Mwankina, kutoka Mtandao wa Watu wenye Ulemavu washio na VVU (NEDPHA); Esther Tibaigana kutoka Kikundi cha Wanawake cha Tushikamane; Janeth Mawinza wa Kikundi cha Wanawake cha Jipange na Mwanaidi Mkwanda kutoka kikundi cha Community Care.
Taarifa iliendelea kwamba: ”Siku moja tu kabla ya kukamatwa zaidi ya wanaharakati 200 wakiwemo waliokamatwa, waliandamana kwa amani kupinga ukimya mrefu wa serikali ambapo mamia ya Watanzania walipoteza maisha kwa kukosa haki yao ya kupata huduma za afya stahili kwa vile serikali ilikosa kuingilia kati na kutatua madai ya madaktari.”
Maandamano hayo yaliyoitishwa kwa ushirikiano wa FemAct, Jukwaa la Katiba, Policy Forum, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na asasi nyinginezo yalimulikwa vyema na vyombo vya habari kwa vile yalifanyika kwenye barabara inayotumiwa na wanasiasa wengi pamoja na viongozi wa serikali na kusababisha msongamano wa takriban masaa mawili.
0 Comments