Makundi ya wapiganaji Sudan Kusini.
Watu wasiopungua 37 wameuawa Sudan Kusini katika upiganaji risasi kwenye mkutano wa amani unaolenga kumaliza ghasia katika eneo hilo, wamesema maafisa.
Maafisa kutoka majimbo matatu walikutana katika mazungumzo yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa katika mji wa Mayendit, kwenye jimbo la Unity, katika jitihada za kupunguza uhasama wa kikabila.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mzozo ulizuka na magari manne kuwasili yakiwa yamejaa polisi ambao mara moja walianza kufyatua risasi.
Miongoni mwa waliokufa ni raia. Wanaharakati wa haki za binaadam wameshutumu ukosefu wa nidhamu miongoni mwa majeshi ya usalama.
Mazungumzo hayo yaliitishwa kufuatia mfululizo wa mapigano, yakiwemo mapigano ambayo watu 74 waliuawa mapema wiki hii.
Mamia ya watu wamekimbia makazi yao kutokana na ghasia hizo.
0 Comments