Top artist wa Tanzania Maarufu kwa jina la chege anategemea kuunguruma Amsterdan tarehe 8 april ambayo ni sikukuu ya pasaka.Akizungumza moja kwa moja na Maganga One Blog kwa njia ya mtandao King James akishirikiana na Eddy kutoka Uganda katika mpango mzima wa show hii kabambe itakayofanyika siku hiyo ya pasaka,King James na Eddy wanawahakikishia ujio huo wa msanii Chege na wanawaomba wapenzi na mashabiki wote wa bongofleva kutoka pande zote za Afrika kuja kushuhudia Chege jinsi gani atakuna nyoyo zenu siku hiyo.Maelezo jinsi ya kufika na kiingilio ni juu ya hiyo picha.tunatanguliza shukrani za dhati kwa kila mmoja atakayekuja kwenye show yetu.
King James & Eddy.