Urusi imeonya kuwa ujumbe wa Kofi Annan, uliotumwa Syria na Umoja wa Mataifa na Jumuia ya Nchi za Kiarabu, unaweza kuwa fursa ya mwisho ya kuepuka vita.
Onyo hilo limetolewa na Rais Dmitri Medvedev wa Urusi, alipokutana na Bwana Annan ambaye amewasili Moscow kujadili swala la Syria, na njia za kumaliza utumiaji nguvu nchini humo.
Anajaribu kuishawishi Urusi - mshirika muhimu wa Syria - ichukue msimamo mkali dhidi ya Rais Bashar al Assad.
Warusi wanasema haifai kuweka muda maalumu kwa Bwana Annan kumaliza kazi yake; na baada ya muda itabainika kama Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linahitaji kuchukua hatua zaidi kuhusu Syria.
Huku nyuma, "Jeshi Huru la Syria" la upinzani, limetangaza kuwa wapinzani watashirikiana katika mapigano yao dhidi ya serikali.
Katika ghasia za karibuni, baina ya askari wa usalama wa Syria na upinzani, wanaharakati wanasema watu kama 54 waliuwawa Jumamosi.
0 Comments