Hawa ni wasichana kutoka Swaziland,mavazi yao na utamaduni wao unajulikana Duniani kote.
Na hawa ni warembo kutoka nchini Kenya,wakenya hawa wana alama zao hasa nembo ya bendera ya nchi yao ambayo upendelea kuiweka katika mavazi yao ili kuonyesha utaifa wao,japo Mlima wa Kilimanjaro sio wao ila ujitangaza kama wao,ieleweke wazi kwamba Mlima Kilimanjaro ni mali ya Tanzania na mlima upo nchini Tanzania.
Hawa ni mabinti wa Kitanzania  kwa Tanzania kuhusu mavazi ya kitaifa hali bado haijawa sawa kwani mpaka leo hakuna vazi rasmi la taifa.
Warembo hawa kutoka Somalia,nao wana mavazi yao rasmi kila ukiwaona tu unajua hawa ni wasomali.
Ukienda South Africa utakutana na hawa mabinti wa Kizulu,South Afrika nao wanamavazi yao ambayo yanatambulika duniani kote.
Zulu boys kutoka South Africa.
Wakina mama wa Kitanzania wakiwa na vazi la Khanga,kwa mfano kama tukipendekeza vazi la taifa liwe khanga hivi kuna ubaya? Maganga One.