Baada ya kimya kirefu na kuondoka bila kuwaaga wapenzi wangu.kwanza nichukue fursa hii kuwaomba radhi kwa usumbufu wote uliojitokeza,nilikuwa likizo ndefuu na yenye utamu kedekede.nimerudi huku mashavu yakiwa yametuna kama unavyojionea hapo juu.ndani ya likizo yangu kuna mengi niliyoyaandaa na miezi michache toka sasa mtayaona.
Naomba tuwe pamoja kwenye kupashana kama kawaida yetu,kwa wale wote walionitumia habari,matukio,mail na mengi mengi nawaomba radhi sana kwa kutowajibu na kutuwarushia habari zao kwenye ukurasa wenu wa Maganga One kutokana na likizo ambayo siwezi kuielezea.nawaomba sana mnisamehe ila mambo kama kawaida yanaendelea.
2 Comments