Sehemu ya Mlipuko ikiendelea na kufuka kwa moshi.
Watu wapatao 200 wathibitishwa kuuwawa kufuatia milipuko katika kambi ya kijeshi katika mji mkuu wa Congo ,Brazzavile.
Mishindo mikubwa ilisikika kilomita kadhaa nje ya mpaka wa Congo hadi mjini Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.Imearifiwa kuwa mamia ya watu walijeruhiwa kutokana na milipuko hiyo.Pichani baadhi ya majeruhi walifikishwa hospitalini hapo baada ya mlipuko huo.
Mwandishi wa BBC Patrice Chieta anasema wengi ya wakaazi wa mashariki mwa Brazzavillle walitoroka majumba yao kufuatia milipuko hiyo.
Anasema milipuko hiyo ilianza majira ya saa mbili asubuhi na ikaendelea hadi mchana.
Wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti mjini Brazzaville wanasema walihesabu maiti 136 huku maiti zaidi zikiendelea kuletwa . Na hospitali nyegine zilizo mjini ziliripotiwa kupokea maiti 70 zaidi.
Akizungumza kupitia Radio ya kitaifa , Waziri wa Ulinzi Charles Zacharie Bowao, alisema milipuko hiyo ilisababishwa ba moto uliotokea katika ghala la kuhifadhia silaha katika kambi ya kijeshi katika eneo la Mpila.
Na baadae Waziri huyo alionekana katika Runinga ya kitaifa akiwasahuri wa Congo Brazzaville wawe na utulivu.
0 Comments