Waziri Mkuu Vladimir Putin ametangaza kuwa ameshinda uchaguzi wa Urais wa Urusi.
Matokeo ya awali yanampa Putin ushindi wa asilimia 60.
Hii inamaanisha kuwa Vladimir Putin anarudi tena kama rais kwa kipindi cha tatu baada ya kuhudumu kama waziri Mkuu wa Urusi.
Kiongozi huo aling'atuko toka kiti cha urais mwaka 2008 baada ya kuhudu kwa mihula miwili kwa mujibu wa katiba ya Urusi.
Putin aliwaambia maelefu ya wafuasi wake kuwa wameshinda katika uchaguzi uliokuwa huru na wa wazi.
Akiandamana na Rais wa sasa wa Urusi ,Dmitry Medvedev kiongozi huyo aliwashukuru wafuasi wao walio kote nchini kwa kujitokeza na kumchagua tena kama rais wao.
Lakini makundi ya upinzani yamedai kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu na kuwa eti kuna baadhi ya watu waliopiga kura mara mbili.
Viongozi hao wa upinzani wametaka watu wajitokeze barabarani kuanzia jumatatu kufanya maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo.
0 Comments