Kijana mmoja ambaye ni raia wa Tibet amejichoma moto jana asubuhi karibu na jengo la Bunge la India kwa kulalamikia ziara ya Rais wa China nchini India.
Kijana huyo ambaye hajajulikana alikimbia umbali wa kama mita 50 huku akiungua kisha kuanguka wakati akishuhudiwa na mamia ya walalamikaji wengine ambao wanapinga utawala wa China juu ya nchi yao ya Tibet.
Kijana huyo alijiwasha mwenyewe kisha kuanza kukimbia karibu na bunge la India lililopo katika mji mkuu wa nchi hiyo.Kijana huyo baadae alpatiwa matibabu ya majereha ya moto katika hospitali ya New Delhi, alisema mmoja wa waandaaji wa Tibet.
Malalamiko hayo yametokea wakati Rais wa China bwana Hu Jintao akiwa anajianda kuitembelea India wiki hii.
Zaidi wa waandamaji 600 wa Tibet wakiwa wamebeba bendera na mabango, waliandamana huko New Delhi mpaka Central Plaza karibu na bunge la India na kuhudhuria mkutano wa maandamano hayo.
Baadhi ya mabango yalisomeka 'Tibet inaungua' na 'Tibet sio sehemu ya China'.
Kiasi cha watu kama 30 huko Tibet walijichoma moto mwaka jana katika kupinga China kuitawala ardhi yao ya Tibet.
0 Comments