Serikali yaTanzania kupitia mamlaka ya vitambulisho NIDA imetenga dola za kimarekani milioni 224 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa vitambulisho vya taifa.
Mradi huu ambao hatua yake ya kwanza itakuwa ni utambuzi na usajili wa raia wake pia utawashirikisha wakimbizi na wageni.
Wataalam mbalimbali hasa wale katika sekta ya uchumi tayari wanatathmini utekelezaji wa mradi huu wa vitambulisho vya taifa ambao ni wa kwanza nchini Tanzania, kuwa huenda ukabadilisha maisha ya raia wa nchi hiyo hasa katika kuwawezesha kupata huduma za kibenki kama vile mikopo.
Kwa mujibu wa mwandishi wetu wa Dar es Salaam Aboubakar Famau aliyezungumza na Dickson Maimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa nchini humo mradi huo utakuwa na hatua kadhaa za utekelezaji.