Vikosi vya serikali Somalia vinavyosaidiwa na majeshi ya Umoja wa Afrika vimeikamata ngome kuu ya wapiganaji wa al-Shabab nchini humo.
"Harakati hii ya kijeshi ni muhimu kurejesha usalama wa Mogadishu" Kamanda wa AU Meja Jenerali Fred Mugisha alisema wakati uvamizi ulipoanza.AU na vikosi vya serikali vilidhibiti sehemu kubwa ya Mogadishu mwaka jana.
Lakini waandishi wanasema wapiganaji wa al-Shabab walifanikiwa kuanzisha mashambulizi katika mji huo kutokea ngome yao ya Maslah.
Al-Shabab wanashambuliwa kutokea sehemu mbalimbali na majeshi ya Kenya na Ethiopia ambayo yameshika kasi hivi karibuni.
Lakini kundi hilo ambalo lilijiunga na al-Qaeda mwezi uliopita bado linadhibiti sehemu kubwa ya kusini na katikati ya Somalia.
Lilielezea kujiondoa Mogadishu mwezi Agosti mwaka jana kama ‘mbinu’ na limeendelea kufanya mashambulizi ya kujitoa muhanga ndani ya mji.
'Sauti za Milipuko'
Majeshi ya serikali ya Somalia yakisaidiwa na vikosi vya AU yalianzisha mashambulizi eneo la Maslah alfajiri, ujumbe wa AU nchini nchini Somlia yamesema katika taarifa.Al-Shabab ilisema inajiondoa kwa hiari kutoka Maslah ambao ni kilometa 5 (maili 3) kaskazini mwa Mogadishu kwenye barabara kuu moja au mbili nje ya mji.
Maafisa kutoka serikali ya mpito inyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na wfanyakazi karibu na ngome hiyo waliiambia BBC Idhaa ya Kisomali kuwa milipuko ilisikika kutoka Maslah wakati wa mapigano.
0 Comments