Waziri mkuu wa Uholanzi akiwa na baiskeli akielekea kazini.tofauti na viongozi wetu wengi wa Afrika ambao hutumia magari ya kifahari na kusababisha msongamano wa magari barabarani.Kiongozi huyu ambaye inasemekana mpaka leo hajaoa na anaishi na mama yake mzazi.wananchi na raia wa Uholanzi hawajali kabisa maisha anayoishi waziri wao,wao wanachojali ni utendaji wa kazi zake kwa wananchi wake.kwa kweli inapendeza sana kuona kiongozi mkubwa kama huyu duniani akiishi maisha ya kawaida na kuwajali wananchi wake kwa vitendo,nasema vitendo kwani mwenyewe binafsi unaweza kuona maendeleo ya nchini Uholanzi.angali baiskeli anayoitumia waziri mkuu huyu,je kwa nchi kama Uholanzi na maendeleo waliyonayo viongozi wetu hawawezi kujifunza kutoka kwa hawa wenzetu?