Yule aliyekuwa mchezaji muziki wa Pakistani ambaye alimwagiwa tidikali mwezi wa Mei mwaka 2000 hatimae amejiua.
Fakhra Younus, 33 amejijiua kwa kujirusha kutoka katika ghorofa ya sita huko Rome nchini Italia baada ya takribani miaka 12 tangu amwagiwe tindikali ambayo mwenyewe alisema imemfanya aonekane kama si binaadamu.
Tukio la kumwagiwa kwa tindikali ambalo inasadikiwa aliyekuwa mumewe, Bilal Khar aliingia nyumbani kwa mama yake mwanamke huyo na kumwagia tindikali Fakhra usoni mwake wakati akiwa amelala.
Unyama huo ambao uliharibu uso wa mrembo huyo na kupelekea kufanyiwa operesheni mara 39 ili kuweka sawa sehemu za uso zilizoharibika. Kutokana na kumwagiwa tindikali hiyo aliunguza nywele zake, alipoteza pua, midomo, sikio la kushoto, kuunguza matiti na hata kupofua moja ya jicho lake.
Younus, kushoto, akiwa na Tehmina Durrani, ambaye alikuwa akimsaidia wakati wa uhai wake
Mwanamke huyo ambaye alifanikiwa kupata mtoto mmoja alihamia Italia kwa matibabu baaday kupata athari hiyo.
Tarehe 17 Machi mwaka huu aliamua kujiua na kuacha ujumbe wa kuwa 'ameamua kujiua baada ya kuona sheria imekaa kimya na baadhi ya watawala wa Pakistani kutokuwa ubinaadamu.
Bilal Khar alikamatwa mwaka 2002 na kufunguliwa mashitaka ya kutaka kuua, lakini aliachiwa kwa dhamana miaka mitano baadae.
Khar ambaye aliwahi kuwa mjumbe katika Bunge na ni mtoto wa gavana ambaye tajiri baadae alichiwa kwa kutokutwa na hatia yoyote, ingawa wengi wa wananchi wanaamini ya kuwa alitumia baadhi ya wanafamilia wake ili kufutiwa madai hayo.
Familia ya Younus wakilia kwa uchungu baada ya mwili wake kuwasili katika uwanja wa ndege wa Karachi nchini Pakistani ukitokea ItaliaMwanamke huyo ambaye alifanikiwa kupata mtoto mmoja alihamia Italia kwa matibabu baaday kupata athari hiyo.
Tarehe 17 Machi mwaka huu aliamua kujiua na kuacha ujumbe wa kuwa 'ameamua kujiua baada ya kuona sheria imekaa kimya na baadhi ya watawala wa Pakistani kutokuwa ubinaadamu.
Bilal Khar alikamatwa mwaka 2002 na kufunguliwa mashitaka ya kutaka kuua, lakini aliachiwa kwa dhamana miaka mitano baadae.
Khar ambaye aliwahi kuwa mjumbe katika Bunge na ni mtoto wa gavana ambaye tajiri baadae alichiwa kwa kutokutwa na hatia yoyote, ingawa wengi wa wananchi wanaamini ya kuwa alitumia baadhi ya wanafamilia wake ili kufutiwa madai hayo.
Mwili wa Fakhra Younus ukitolewa nje ya uwanja wa ndege wa Karachi baada ya kuwasili ukitokea Italia
0 Comments