Mkurugenzi wa Uhusiano na Kitengo cha Sheria wa TBL, Steve Kilindo, akitoa maelezo kwa Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha Anga kuhusu historia ya kampuni hiyo.
Meneja wa Masuala ya Usalama mahali pa kazi wa TBL, Renatus Nyanda, akielezea kuhusu hatua mbalimbali za uzalishaji wa bia kiwandani hapo.
Meneja Ubora wa Bidhaa za TBL, Lydia Soi akitoa maelezo jinsi wanavyodhibiti ubora wa bidhaa kiwandani hapo.
Ofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kikosi cha Anga, akielekezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni yaYour Solution Tanzania Limited, Damian George, jinsi ya kukitumia kifaa cha kisasa cha kuzimia moto kiitwacho DSPA, walipotembelea kiwanda cha bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kujifunza masuala ya usalama kazini, afya za wafanyakazi na utunzaji wa mazingira.
Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kikosi cha Anga, wakitembelea kiwanda cha bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, sehemu ya matanki yanayotumika kuchachulia bia.
Askari hao walifanya ziara ya kujifunza masuala ya usalama kazini, afya kwa wafanyakazi na mazingira.Askari wakiangalia unga wa mahindi unaotumika kutengenezea bia.