Wanamgambo wa Taleban
Vijana waingereza wenye asili ya kiafrika, huenda wakawekwa kasumba na Al-qaeeda wakati kundi hilo likitafuta kukita mizizi barani Afrika.
Taarifa hii imetolewa na kundi la wataalamu wa maswala ya dunia wanaosema kuwa Al-qaeeda inatafuta kuweza kujikwamua kutokana na vita dhidi ya kundi hilo.
Kulingana na wataalamu, hali kama hiyo inaweza kusabisha changamoto kubwa kwa Uingereza pamoja na mashirika mengine ya kijasusi katika chi za magharibi.
wanaonya kuwa vijana walio katika tishio la kushinikizwa zaidi kimawazo kwa kufunzwa siasa kali ni wenye asili ya kisomali pamoja na wengine kutoka nchi za Afrika mashariki na Magharibi.
Serikali ya Uingereza imesema kuwa inakabiliana na tisho la ugaidi ndani ya nchi hiyo
Katika miaka kumi na tano iliyopita vijana kutoka Pakistan, wale wenye asili ya kiafrika, na hata wahindi wanaoishi nchini humo, wameweza kushinikizwa na kufunzwa siasa kali kulingana na ripoti iliyochapishwa na taasisi ya Royal United Services.