Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt,Pamela Kikuli (katikati) akiongea na waandishi wa habari (wahapo pichani) wakati wa kutangaza Tuzo ya dhahabu yenye hadhi ya juu zaidi ya ubora wa bidhaa za kimataifa ijulikanayo kama “Grand Gold Quality Award” waliyoipata kwa mara ya pili sasa,kwenye mkutano uliofanyika leo kwenye ukimbi wa Mikutano wa TBL jijini Dar es Salaam.Kulia ni Meneja wa Mambo ya Nje na Mawasiliano wa TBL,Emma Orio na Kushoto ni Mpishi Mkuu wa Bia wa TBL,Mzee Gaudence Mkolwe.
Bia ya Ndovu Special Malt inayotengenezwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), imedhihirisha ubora wake kimataifa baada ya kushinda kwa mara nyingine tena tuzo ya dhahabu yenye hadhi ya juu zaidi ya ubora wa bidhaa kimataifa ijulikanayo kama “Grand Gold Quality Award”
Akizungumza na waandishi wa habari, meneja wa Bia ya Ndovu Bi. Pamela Kikuli alisema; Tunayo furaha kubwa sana kuwajulisha wadau wa Bia hii ya Ndovu Special Malt juu ya ushindi huu mkubwa ambao Bia hii imenyakua katika tuzo za bidhaa za kimataifa zinazotolewa na Taasisi ya kimataifa inayoangalia ubora wa bidhaa ya “Monde Selection International Quality Institute” iliyopo Brussels, Ubelgiji (Belgium).
Tuzo hii yenye hadhi ya juu kabisa katika ubora wa bidhaa kimataifa inajulikana kama “Grand Gold Quality Award” na hushindanisha bidhaa toka Mataifa mbalimbali ambapo mwezi huu Aprili taasisi hiyo imetangaza rasmi kuwa “Ndovu Special Malt” imeshinda tena tuzo ya “Grand Gold” kwa mwaka 2012. Alisema Pamela.
Akizungumzia Ubora wa bia ya Ndovu Special Malt, Mpishi mkuu wa Bia wa TBL Bwn. Gaudence Mkolwe alisema; Tunakumbuka kuwa mwaka 2010 Bia hii ya Ndovu Special Malt ilishinda kwa mara ya kwanza tuzo hii ya Grand Gold ikiwa na umri wa miezi tisa tu sokoni toka ibuniwe, na kuweka historia kwa nchi yetu kuwa ndio Bia ya kwanza kushinda tuzo hiyo hapa Tanzania, na leo Bia ya Ndovu Special Malt inawadhihirishia wadau wake na watanzania wote kwa ujumla kuwa imeendeleza ubora wake kitaifa na kimataifa hadi kupata tuzo hii kwa mara ya pili.
Haya ni mafanikio makubwa na ya kujivunia si tu kwa wapenzi wa Bia hii, bali kwa Taifa zima kwa kuwa na bidhaa zinazotingisha anga za kimataifa kwa Ubora, na ukizingatia kuwa Bia hii imebuniwa na watanzania na inatengenezwa na watanzania. Haya ni mafanikio makubwa ya kujivunia.
Nae Meneja wa miradi maalum na Mawasiliano wa TBL Bi. Emma Oriyo alitoa utaratibu wa upokeaji wa tuzo hizo; Tuzo hizi za mwaka 2012, zitakabidhiwa rasmi mwezi Juni 2012 katika hafla kubwa iliyoandaliwa huko Athens, Ugiriki na kufuatiwa na hafla mbalimbali zitakazofanyika hapa nyumbani mara tu tuzo hii itakapowasili nchini.
Tunawapongeza wapenzi wote wa Bia hii ya Ndovu Special Malt, kwa kufanya chaguo sahihi kwa kutumia Bia inayoongoza kwa ubora wenye hadhi ya juu na tunawaahidi kuendelea kuwapatia ubora huu siku zote. Alisema Bi. Emma.
0 Comments