Mpango mzima ulikwenda kama unavyojionea,yani ni full mzukaa Chege aliwakonga mashabiki kiukweli
Mkono mmoja weka juu kila mmoja aliiimba kama jinsi Chege anataka aimbe basi ilikuwa ni balaaaa...!!!
King James mwenye koti jeusi akiusikilizia muziki wa Chege na nyuma yake brother Mnyenga akitabasamu kwa furaha.
Yaani ni Full Mzuka.....!!!
Kwa kudhihirisha kuwa bongo fleva ni mziki unaotambulika duniani na Chege ni kipenzi cha watu kila taifa lilikuja kumshuhudia kijana Chege.
Kutoka kushoto ni Bidada mama Kiza,King James na mke wa King James(Mrs James)
Black is Always Beauty.....hawa ni madada waliofika kwenye show ya Chege
Waaaawwwooo!!! ni Brandina Kulia akiwa na mashoga zake waliopendeza vyema kwenye show ya kijana Chege.
Wanaume wakiwa na mwanaume Chege
Aisee Chege anapendwa na wengi maana kila mmoja alipenda kumpa sapoti na hii kwa kweli niliipenda sana ukumbini hapo.
Watu walipendeza sana ukumbini na hata ukipiga picha unapenda kuiangalia
Brother Nyembo na mkewe kipenzi walipata kumbukumbu ukumbini hapo...Nice Picture!!
Aaaah bwana mdogo Yusuf akiwa na bi mdogo .............hapo yani mambo dushelele..!!
Raha ya picha ni pale kuona watu wamependeza kama hivii,show ya Chege ilijaza watu wengi na kila mmoja alikuwa amependeza kisawasawa
Mashosti wa nchi mbalimbali walikuwa wameketi wakiangalia show ya kijana toka tmk Chege Chigunda mtoto wa mama Said.
Nani hasiyemjua King James? hapo King James akiwa na Chege kabla ya kuanza kwa show
Mke wa James kushoto akiwa na shoga yake kipenzi wakipata mambo fulani ya Flash
Wakati Chege anakamua vilivyo jukwaani kuna walioshindwa kujizuia na kupanda kwenye stage na kujumuika katika kukata mapanga ya Tmk,pichani bidada akiwa na chege kwa makamuzi
Ukiachilia mbali ya show ya Chege,kuna show kibaooo za utangulizi ziliburudisha watu.
Nyuma ya pazia mambo yalikuwa hiviiiiiii,hapo ni mimi na Chege tukihojiana yani ilikuwa full kucheka. |
0 Comments