Askari wa usalama wa Guinea-Bissau wamevunja maandamano ya kutaka waziri mkuu aliyekamatwa katika mapinduzi ya Alhamisi, aachiliwe huru.
Waandamanaji kadha wamejeruhiwa.
Waziri Mkuu, Carlos Gomes Junior, alikuwa akiongoza katika kampeni za uchaguzi, ambao ulipangwa kufanywa mwezi huu.
Inafikiriwa Bwana Gomes amepelekwa kwenye kambi ya jeshi mjini Bissau, pamoja na rais wa mpito, Raimundo Pereira.
0 Comments