Kutokana na hofu hiyo, wanachuo wameshauriwa kutembea kwa makundi kwa lengo la kujihami na wahuni hao.
Hayo yamethibitishwa na Msemaji wa Chuo hicho, Karim Meshack, aliyekiri kuwa waporaji hao ni tishio katika eneo hilo, kiasi cha kushauri wanafunzi kutembea kwa makundi ya watu watano hadi sita.
Meshack alikuwa anathibitisha habari ambazo gazeti hili lilizipata zikidai kuwa, kuna matukio kadhaa ya uporaji, huku baadhi ya wanafunzi wa kiume wakidaiwa kuporwa mali na kulawitiwa.
“Ni kweli katika siku za katikati kulikuwa na matukio ya wanafunzi kupigwa na kuporwa vitu kama simu, lakini hayo mengine nami nayasikia juu juu,” alisema.
Hata hivyo, mmoja wa wanafunzi wa Chuo hicho alidokeza kuwa, kutokana na hofu ya vibaka na matukio mengine wa makundi ya watu wasiofahamika, kasi ya mahudhurio ya watu wanaojisomea nyakati za jioni imepungua
“Zamani ikifika saa moja au mbili wanafunzi kibao wanajazana kwenye ‘mdigrii’, lakini sasa ikifika saa mbili wanafunzi wanakuwa wa kuhesabu kutokana na kila mmoja kuwahi kurudi anakoishi kwa kuogopa vibaka,” alisema.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen, alipoulizwa juu ya matukio hayo, alisema hana taarifa kwa kuwa hakuna tukio lililoripotiwa.
“Kama kuna matukio yaripotiwe ili uchunguzi ufanyike na wahusika watafutwe na kuchukuliwa hatua,” alisema huku akiwataka wananchi kuwa na tabia ya kutoa taarifa za vitendo vya uhalifu ili wahusika wabainike na kukamatwa na si kukaa kimya.
Diwani wa Kikuyu Kaskazini, Johnick Kisasi, alisema kuwa kumekuwa na tabia ya wananchi kushindwa kutoa taarifa za vitendo kwa kihalifu katika Serikali za Mitaa hali ambayo inafanya wahusika washindwe kuchukuliwa hatua.
“Matukio yapo, lakini hakuna taarifa rasmi kuwa wamefanyiwa vitendo hivyo, ila ni kweli tunasikia wanafunzi walilawitiwa na mwingine kuvuliwa nguo, sasa kama waliofanyiwa vitendo hivyo wameamua kuwa kimya, sisi hatutakuwa na taarifa rasmi,” alisema. Alikiri kuwa vitendo vya kihalifu vimekithiri katika kata hiyo na juhudi zinahitajika ili kufanya eneo hilo kuwa salama kama ilivyokuwa siku za nyuma. Imeelezwa kuwa, moja ya mbinu zinazotumiwa na vibaka hao nyakati za usiku ni kupanda juu ya miti kwa lengo la kuwavizia wapita njia na pindi wanapokaribia maficho yao, hushuka na kudhuru watu wasio na hatia. source. |
0 Comments