Na Wilbert Molandi
LAZIMA akae mtu! Hivi ndivyo utakavyoweza kusema kwenye pambano la ngumi kuwania ubingwa wa Super Middle wa Shirikisho la Ngumi Dunia (IBF), kati ya Francis Cheka na Mada Maugo kesho Jumamosi kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba jijini Dar.
Pambano hilo litakalokuwa la raundi 12 linatarajiwa kumaliza ubishi baada ya Maugo kupokea kichapo mara mbili kutoka kwa mpinzani wake huyo.
Mratibu wa pambano hilo ambalo mshindi atapata gari aina ya Toyota Corolla 111, Kaike Siraji, amesema maandalizi yote yanaendelea vizuri na gari lipo tayari kukabidhiwa kwa mshindi.
Alisema kutakuwa na mapambano saba ya utangulizi ambapo ni kati ya Cosmas Cheka vs Mumba, Amosi Mwanakana vs Ramadhani Shauri, Moro Best vs Nasibu Ramadhani, Asha Ngedere vs Salima Kihombwa, Jamila Matimbwa vs Mariam Abdalah na Said Mberwa vs Ibrahim Marokorwa.
Viingilio vya pambano hilo ni shiligni 10,000 kwa viti vya VIP na 5,000 kwa viti vya kawaida. Wakati huo huo, Francis Cheka amesaini mkataba wa kuzichapa na Japhet Kaseba mnamo Julai 7, mwaka huu, katika pambano la raundi 12 litakalofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.