Wanamuziki wa Pah One walipotembea ofisi za Global Publishers wakiwa na kimwana Wema Sepetu aliyekuwa miongoni mwa watu waliowapokea.
Wema Sepetu akiwa amepozi katika ofisi za Global baada ya kuwapokea Pah One.
KUNDI la muziki la Pah One kutoka Afrika Kusini ambalo litatumbuiza Jumapili hii katika kituo cha maraha cha Dar Live huko Mbagala jijini Dar es Salaam tarehe 29 Aprili, limewasili nchini na liko tayari kufanya shoo kali kwa kushirikiana na mwanamuziki nyota nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond’ ambaye atatua katika sehemu hiyo kwa kutumia helikopta.