Aisee hapo chini unachokiona ni kofia ya afisa wa polisi ikiwa imemtoka kichwani kwa vishindo vya pale uwanjani jinsi walivyokuwa wakipita kutoa heshima kwa rais.
Mr President akimsalimia First Lady ambaye ni mkewe mama Salma Kikwete uwanjani hapo,japo walikuja pamoja ila heshima na upendo kwa mkewe inanipa raha sana mimi Maganga One.Hongera sana Muheshimiwa Rais kwa mapenzi unayoyaonyesha kwa mkeo mbele za watu. 
Wapenzi wasomaji,mnapopata picha na habari kwenye magazeti,mitandao na kwengineko msifikiri watu wanazipata kirahisi...ebu angalia wanaume wa shoka jinsi wanavyonasa taswira za matukio ndipo ujue kwamba kuna kazi ya ziada kwa watu hawa.Hongereni sana wanahabari wenzangu kwa kazi nzuri kama hii.