Huwezi kuamini jinsi umati wa watu ambao kila mmoja anataka kuona au kusikia kuhusu kifo cha msanii Steven Kanumba.
Njiani barabara zimekuwa tabu kupitika kabisa kutokana na hali ya umati wa watu jinsi ulivyojaaa kwa kusikia msiba wa kijana Steven Kanumba
Jamani msiba huu ni mzito kwa kila mmoja aliyesikia juu ya mauti ya kijana huyu Kanumba.
Ray Kigosi(mwenye kofia) msanii wa filamu za Kitanzania ambaye alifika kwenye msiba huo na wasanii wengine
Viongozi mbalimbali wa serikali walifika kuomboleza msiba huo
Mbunge wa Kinondoni Mh:Iddi Azan nae alifika kwenye msiba huo kuomboleza pamoja na wananchi wake.
Mwenye shati la njano na blue ni Kiongozi wa magazeti ya global publisher Ndugu Eric Shigongo ambaye nae aliwasiri kwenye msiba kuomboleza na wananchi wa Tanzania.(picha zote toka Michuzi)
SALAMU ZANGU ZA RAMBIRAMBI KUHUSU KIFO CHA MSANII STEVEN KANUMBA
Ndugu watanzania na wasanii
Kwa niaba yangu na familia yangu kwa ujumla nachukua fulsa hii kuwapa pole wazazi, ndugu,jamaa na marafiki wa karibu wa msanii Steven Kanumba ambaye alifariki usiku wa kuamkia leo.kwa kuwa si rahisi kuamini au kusikia kwamba kijana huyu mtanashati na mcheshi kwamba amefariki,ila hatuna budi kukubaliana na tunachokisikia.
Nikiwa nchini Holland likizo nimepokea habari hizi kwa mshtuko mkubwa sana ila kwa kuwa sina jinsi lazima nikubaliane na matokeo ya kifo hicho.Steven Kanumba kijana aliyejizolea sifa kemkem kutokana na shughuli zake za sanaa ya filamu ndani na nje ya nchi kwa ubora na uzuri wa kazi hizo kwa kweli ametuachia pengo kubwa sana na kuzibika kwake itakuwa ni shughuli sana.
Nawaomba wasanii wenzake na wananchi kwa ujumla kumuombea kijana huyo Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Steven Kanumba mahala pema peponi.tukumbuke kwamba yeye ametangulia na sisi tunafuata.
Maganga One - Blogger.
07 April 2012,Den Haag
Holland.
0 Comments