Kila mmoja ameshikilia mto na kuanza kupigana na mwenziwe,kiukweli jamani huu ni mchezo ambao ndio kwanza nimeuona maishani kwangu,maana nakumbuka enzi hizoo tulikuwa tukicheza  na wadogo zangu chumbani na ikitokea mto umechanika basi hapo mjiandae kucharazwa bakora
Maganga One nikafika eneo la tukio kama mnavyoniona ili nipate cha kuwaletea waungwana mjionee nanyi.
Nikatoa kitochi changu cha mchina ili nikamate taswira
Huku patashika inaendelea tu,yani vurugu mtindo mmoja kila mmoja anajitahidi kupambana anavyoona yeye
Mie nikaseti vyema kitochi changu cha mchina ili niwanase vyema wahusika
Nikawa naangaika kuweka engo sawa ili nipate picha vyema,maana kulikuwa na watu kibaoo na paparazi ndio usiseme
Nikamaliza kazi yangu nikaona aah acha nirudishe kitochi changu kwenye begi mie,huku kushoto kwangu polisi akiwa makini kabisa kuhakikisha usalama kwa raia na washiriki wa mapigano ya mito hawapati matatizo yoyote
Kama picha za kuwaonyesha watu wangu nimeshazipata kwanini niendelee kubaki pale? nikaona aah acha nijikate taratibu muungwana mie.watu wangu mnasemaje kuhusu hii kali ya kupigana na mito na sisi tuianzishe nini ? kazi kwenu..